ASSAs

MANENO ALIYOYAONGEA MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE,LEO

924
0
Share:

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimezindua mfumo wake mpya wa Kidigitali wa uendeshaji wa Chama hicho ambapo kitakuwa kikikusanya ada za Unachama wa wanachama wake na kukifanya kujitegemea.

Mwenyekiti CHADEMA Taifa Freeman Mbowe

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama  hicho uliofanyika leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, amesema mfumo utawasaidia kukusanya karibia Bilioni 5 kwa mwaka.

Mbowe amesema “Leo tunazindua mfumo wa Kidigitali tutahama kutoka Analog tutahamia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, tunahitaji kujenga chama kitakachojitegemea, kwa sababu Serikali inafikiri chama hichi kinategemea sana Ruzuku”

Aidha Mbiwe amesema kuwa “Hatutambui Uchaguzi wowote uliofanyika wa Serikali za Mitaa, kokote ambako wagombea walikuwepo watengeneze Serikali Vivuli kuangalia matatizo ya wananchi

(Visited 164 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us