ASSAs

TETESI ZA SOKA JUMATANO DISEMBA 18, 2019

1175
0
Share:
Paul Pogba

Real Madrid wanamnyemelea Paul Pogba

Manchester United hawatamruhusu kiungo wao Mfaransa Paul Pogba, 26, kuihama klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Mail)

United inaamini kuwa itamsajili mshambuliaji nyota wa Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland kwa kitita cha pauni milioni 76 mwezi Januari – na endapo wataruhusu mchezaji huyo asalie kwa mkopo Salzburg mpaka mwisho wa msimu. (Sun)

Hata hivyo klabu ya Red Bull Leipzig pia wamempatia ofa mpya kwa minajili ya kumshawishi mshambuliaji huyo mwenye 19 kusalia klabuni hapo. (Kicker, via Mail)

Haaland
Image captionHaaland (kushoto) ni moja ya washambuliaji hatari zaidi Ulaya kwa sasa

Carlo Ancelotti atambakiza kocha wa muda wa Everton Duncan Ferguson kama sehemu ya benchi la ufundi kama atateuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo. (Telegraph)

Ajenti wa Cristiano Ronaldo, bwana Jorge Mendes amedokeza kuwa nyota huyo mwenye miaka 34 huenda akamaliza maisha yake ya kandanda katika klabu ya Juventus. (Sky Sports, via Goal)

Manchester City wamewapiku Manchester United katika mbio za kutaka kumsajili beki kinda wa Barcelona Juan Larios, 16, mwezi Januari. (Record)

Kante
Image captionKante amekuwa akihusishwa na uhamisho kuelekea Barcelona

Barcelona hawana mipango ya kumsajili kiungo mkabaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa N’Golo Kante, 28. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Klabu za Ligi ya Primia Liverpool, Manchester United na Chelsea wamepatwa na pigo baada ya winga raia wa Ujerumani Kai Havertz, 20, kubainisha kuwa anataka kubaki katika klabu yake ya Bayer Leverkusen inayoshiriki ligi ya Bundesliga. (Sky Sports)

Crystal Palace wataendelea kumthaminisha mshambuliaji wao raia wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Mail)

Kocha wa zamani wa Newcastle na Liverpool Rafa Benitez, ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Uchina ya Dalian Yifang, amesema ipo siku atarejea Ligi ya Primia. (The Athletic)

(Visited 499 times, 1 visits today)
Share this post