ASSAs

GUMZO TENA KWA MAMA DIAMOND

1580
0
Share:

Mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ameibua gumzo mtandaoni baada ya picha yake kusambaa akiwa amebebwa kimahaba na mumewe, Ramadhan Abdul ‘Shamte’

Picha hiyo inayomuonesha mama Diamond akiwa amebebwa na Shamte, ilisambaa katika mtandao wa kijamii wa Instagram huku watu wengine wakisema ni aibu kwa mama kama huyo kupiga picha za aina hiyo.

“Duh, Mungu wangu! Hii sasa ni shida mpaka naona aibu licha ya kwamba picha imepigwa na mtu mwingine, lakini aibu naiona mimi. Inakuwaje mama mwenye mtoto mkubwa kama Diamond, tena staa kufanya hivi, mwanaye sijui huwa anajisikiaje,” aliandika mfuasi mmoja kwenye mtandao huo wa Instagram.

(Visited 300 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us