ASSAs

LIGI YA UVCCM WILAYA YA SIHA YAFIKIA TAMATI KWA KISHINDO

330
0
Share:

UMOJA WA CHAMA CHA MAPINDUZI LIGI WILAYA YA SIHA YAFIKIA TAMATI LEO

24.12.2019

Kutokea Tarehe 13.12.2019 Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Siha Ndugu Wilson Mushi Alipozindua Mashindano Haya ya Mchezo wa Mpira wa Miguu Wilayani Siha Ambapo yalihusisha Jumla ya Timu 18 Zilizotoka Katika Kata 17 Pamoja na Timu ya Jeshi la Polisi Iliyokamilisha Timu 18 Jumla.

Leo Yamefika Tamati Kwa Timu ya Uvccm Kata ya Sanya Kuigalagaza Timu ya Uvccm Kata ya Nasai Kwa Gori 5-2.
Mgeni Rasmi Aliyefunga Mashindano Hayo alikuwa Ni Katibu Wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Kilimanjaro Ndugu Jonathan Mabihya Ambapo Alisema Machache,

“Wapo Watu Walikuwa Wanasema Kanda ya Kaskazini Imebaguliwa Lakini Nataka Niwaambie Chama cha Mapinduzi Chini ya Dr John Pombe Joseph Magufuli Mkoa wa Kilimanjaro Ni Mashahidi Mnaona Mabarabara , Mahospitali , Mashule , Na Sasa Usafiri wa Uhakika wa Treni.”Katibu CCM Mkoa Kilimanjaro Ndugu Jonathan Mabihya.

“Ninyi Kama Vijana Lazima Mjitahidi Kushiriki Katika Kukuza Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja Kupitia Vikundi Ambavyo Mtakopeshwa Na Halmashauri Kama 4% kwa Vijana.” Katibu CCM Kilimanjaro Ndugu Jonathan Mabihya.

“Michezo Isihishie Kwenye Burudani Pekee Ni Lazima Tutumie Michezo Kama Ajira Wapo Wachezaji Wameajiliwa na Vilabu Mbali Mbali Hapa Nchini” Katibu CCM Kilimanjaro Ndugu Jonathan Mabihya.

Aidha Mgeni Rasmi Aliweza Kumkabidhi Mshindi wa Kwanza Zawadi ya Ng’ombe , Medali Pamoja na Kikombe , Lakini Mshindi Wa Pili Akijiondokea na Jezi Seti Moja Pamoja na Medali.

Fainali Iyo Ilihudhuliwa na Mbunge wa Jimbo la Siha , Katibu Mwenezi Wa CCM (W) Siha ,Wajumbe wa Halmashauri ya Wilaua na Viongozi wa Chama Na Jumuia Kutoka Kutoka Kata Mbali Mbali.

Tukutane Kazini.

Imetolewa na
Katibu Hamasa (W) Siha.

(Visited 34 times, 1 visits today)
Share this post