ASSAs

GIGY MONEY ALAANIWA NA MAMA YAKE”Hata nikifa asinizike”

1893
0
Share:

Mama mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, Fatuma Katunda ‘Kissa’ amemlaani mwanaye huyo na kufikia hatua ya kusema asimzike kutokana na kumtukana sana.

Mama Gigy alisema hivi karibuni mwanaye huyo alikwenda nyumbani kwake maeneo ya Keko-Akida, Dar na kumporomoshea matusi ya nguoni kisa ugonjwa wa mwanaye, Maryan.

“Alichonifanyia Gigy sitaki hata kumuona, nilikuwa ninaishi na mtoto wake Maryan kutokana na kazi zake kuwa hazitabiriki, sasa Gigy alikuja nyumbani kwangu Keko akamkuta mtoto anaumwa kwa sababu ana pumu ya ngozi.

“Hapo ndipo alipoanza kunitukana matusi ya nguoni akidai kwamba nimeshindwa kumuhudumia mtoto wake vizuri mpaka akaugua.”

“Nikamwambia nimeshampeleka hospitali na anatumia dawa, hakutaka kunielewa akaendelea kunitukana. Ikabidi nimwambie simtaki siyo mwanangu maana mtoto anayemjua mama hawezi kumtukana kiasi kile.”

“Akanijibu kuwa anatafuta mama mwingine, kwa hiyo yeye atafute huyo mama mwingine na mimi hata nikifa asinizike,” alisema mama Gigy.

(Visited 929 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us