ASSAs

JPM AWASILISHA FOMU ZA TAMKO LA MALI

505
0
Share:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewasilisha tamko linalohusu Mapato, Rasilimali na Madeni ya viongozi katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria na kikatiba.

Tamko hilo limewasilishwa katika Ofisi za Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Katibu wa Rais, Bwana Ngusa Samike ambaye ametumwa na Mhe Rais akiwa mapumzikoni Chato na kupokelewa na Kamishna wa Sektretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Harold Nsekela.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupokea tamko hilo Jaji mstaafu Nsekela amesema kitendo alichokifanya Mhe.Rais kimetekeleza takwa la kikatiba Ibara ya 132 (5) (D) linalowataka viongozi kuwasilisha taarifa za tamko la mapato, rasilimali na madeni mara kwa mara lakini pia ametekeleza sheria no 13 ya mwaka 1995 kingu cha 9.

(Visited 53 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us