ASSAs

AGIZO LA DKT. BASHIRU ALLY KWA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI

155
0
Share:

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt Bashiru Ally, amewataka wanachama wa chama hicho kuacha siasa za kuabudu watu badala ya chama, kwani kufanya hivyo ni kutekeleza siasa za kishirikina. 

Dkt Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Mabalozi na viongozi wengine wa chama hicho, katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.

“Kuabudu watu ni ushirikina, wanaotaka kutukuzwa na kujifanya wao ndio wanaweza mambo, wanafanya siasa za kishirikina” amesema Dkt Bashiru.

Aidha amewataka kuacha kufanyiana fitina ndani ya chama kwa kuwa fitina zina malipo yake, “Siwezi kuwazuia kunywa sumu kama mmeamua kufanya hivyo, lakini siwezi kuogopa kuongea ukweli” amesema Dkt Bashiru.

(Visited 17 times, 1 visits today)
Share this post