ASSAs

DIAMOND AMPONZA KAKA WA ALLY KIBA, ASIMULIA HAYA

1713
0
Share:

Kaka yake na alikiba anayejulikana kwa jina la Issa Azam ambaye wamekuwa wote na Alikiba tangu utotoni katika mtaa wa Hombo mkoani Kigoma licha ya yeye kwa sasa kufanyia kazi zake Dar Es Salaam amefungukla mwanzo mwisho kuhusu Alikiba ambao walilelewa nyumba moja kabla ya Alikiba kuja Dar kwa Wazazi wake na kuanza harakati za Maisha.

Akiwa shabiki mkubwa wa Diamond anasema kuwa mwanzo kabisa alikuwa anawashabikia wote lakini tatizo lilianza pale Alikiba na Diamond walipotofautiana na yeye hakuwa na namna ilibidi afuate moyo wake unatakaje na moyo wake ulikuwa unamkubali sana Diamond kuliko Alikiba hasa yale majigambo ya Diamond na upambanaji wake.

Issa anaongeza kuwa ndugu zake walianza kumtenga baada ya kuona kuwa hamshabikii Alikiba ambaye ni ndugu yake na badala yake yeye anamshabikia Diamond ambaye sio ndugu yake kwa maana nyingine alionekana msalitti ndani ya familia.

Issa aliendelea kuongea na kusema alishawahi kupigwa mara mbili na mashabiki wa Alikiba hadi kuumizwa vibaya na hapo ndipo Diamond aliposikia na kuanza kuwa nae karibu, lakini baadaye sana famililia ilikuja kuona haya ni mambo ya vijana ni kama watu kutoka familia moja kushabikia timu tofautitofauti kama vile ndugu wanaweza kupishana wengine kushabikia Simba na wengine kushabikia Yanga.

(Visited 326 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us