ASSAs

MTOTO AUAWA, ACHUNWA NGOZI NA KUKATWA NYETI

398
0
Share:

Mtoto Hassan Muba mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Kibiti, mkoani Pwani, anadaiwa kuuawa kisha kuchunwa ngozi usoni na watu wasiojulikana huku ikiripotiwa pia kuondolewa sehemu zake za siri.

Kwa mujibu wa habari zilizopo,  Hassan alipotea Januari 7, mwaka huu,  na kupatikana siku mbili baadaye, Januari 9 chini ya mwembe.

“Tulikuta nguo ziko pembeni, amechunwa ngozi usoni na ameondolewa sehemu za siri, amekatwa nyama makalioni na mapajani, shingo imevunjwa pia,” alisema Mohammedi Pepe katika mahojiano.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga, akizungumzia tukio hilo alisema: “Ni kweli taarifa tunazo lakini tumefanya uchunguzi na kubaini hakuondolewa sehemu za siri isipokuwa zilisinyaa.”

(Visited 33 times, 1 visits today)
Share this post