ASSAs

MWANAFUNZI ALIYEPATA DIV 1 YA 7 ALIYEFARIKI AKITOKA KUTAZAMA MATOKEO, AZIKWA

1095
0
Share:

Mwanafunzi Honest Mulokozi Juventus aliyefariki dunia wakati akitoka kutazama matokeo yake ya kidato cha pili, amezikwa kijijini kwao Wilaya ya Karagwe Jimbo Katokiki la Kayanga.

Honest aliyekuwa akisoma katika Seminari ya Rubya iliyopo Parokia ya Kasambya, Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera, alifariki dunia wakati akitoka kutazama matokeo yake ya kidato cha pili, maeneo ya Shule ya Optima akiwa anaendesha pikipiki baada ya kugongwa na gari la mizigo.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Januari 9, 2020, na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt. Charles Msonde, Honest alikuwa amepata ‘Division One’ ya pointi 7 kwa maana ya alama ‘A’ kwa kila somo alilofanya mtihani huo.

Matokeo yake ya FTNA:

Civics = A
History = A
Geography = A
B/Knowledge = B
Kiswahili = A
English = A
Physics = A
Chemistry = A
Biology = A
B/Maths = A

Division One (Points 7).

Tumuombee apumzike kwa amani. Raha ya milele umpe Ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani!

(Visited 506 times, 1 visits today)
Share this post