ASSAs

IRAN YAKANA KUWASHAMBULIA WAANDAMANAJI

253
0
Share:

Polisi nchini Iran katika mji mkuu Tehran, wamekanusha kutumia silaha dhidi ya waandamanaji walioghadhabishwa na kudunguliwa kwa ndege ya Ukraine.

Maafisa wa polisi walikuwa wamepata maagizo ya kuonyesha kwamba wao imara, mkuu wa polisi amesema.

Video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili, zilirekodi kile kilichoonekana kama maafisa wakifyatua risasi pamoja na mwanamke aliyejeruhiwa akibebwa.

Maandamano yalianza Jumatatu baada ya Iran kukubali kwamba ilirusha kombora kimakosa dhidi ya ndege ya abiria ya Ukraine na kuanguka karibu na Tehran.

Watu wote 179 waliokuwa kwenye ndege hiyo PS752, wengi wao wakiwa raia wa Iran na Canada walikufa.

ShambulioHaki miliki ya pichaAFP
Image caption
Hakuna abiria hata mmoja aliyeripotiwa kupona
Siku tatu za kwanza baada ya kutokea kwa ajali, Iran ilikanusha kwamba vikosi vyake vimedungua ndege hiyo na kusema kwamba ilipata matatizo ya kiufundi.

Hata hivyo, ilikubali kudungua ndege hiyo baada ya video kuonyesha kombora likipiga ndege hiyo, na kusababisha hasira kote nchini Iran.

(Visited 24 times, 1 visits today)
Share this post