ASSAs

TECNO YAIMARISHA USHIRIKIANO WAKE NA GOOGLE 2020

334
0
Share:

Kampuni ya Simu ya TECNO Yaimarisha Ushirikiano wake na Google Kwenye Mkutano wa Maonesho ya Teknolojia 2020

Toleo jipya la simu CAMON 12 Pro ya hivi karibuni imewekewa  kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) ambacho kinaruhusu watumiaji kufanya mambo mengi zaidi kwenye mfumo wa Google.

Kampuni kinara ya Kimataifa ya simu za rununu ya TECNO yenye simujanja yake  ya  Camon 12 Pro ya hivi karibuni, inayowezeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Pie ya Google (Google’s Android™ 9 Pie operating system), imeweka kitufe cha Msaidizi wa Google (Google assistant) kwenye CAMON 12 Pro katika mkutano wa maonesho ya teknolojia ya mwaka 2020 Januari hii.

TECNO imejiunga na kuwa mshirika  wa Google kuleta mfumo mpya wa uendeshaji kwa wateja wake. Wakati Google inafanya maboresho ya mfumo endeshi (Android) kwaajili ya kuleta ufanisi madhubuti kwenye vifaa janja vipya vya kisasa, TECNO ilizindua simu mpya ya kisasa ya CAMON 12 Pro kwa kuweka Kitufe cha Google assistant  ambayo ilioneshwa kwenye kibanda cha Google katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020 ili kusaidia watumiaji kufanya mambo kwa haraka zaidi na kupangilia vitu muhimu kwenye ratiba ambavyo vinavyoweza kufanyika baadaye.

Google ikionesha Simujanja zenye kitufe cha Google Assistant kwenye banda lake katika mkutano wa maonesho ya teknolojia 2020.

(Visited 38 times, 1 visits today)
Share this post