ASSAs

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UJERUMANI ATOA NENO KWA IRAN

224
0
Share:

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Heiko Maas amefanya ziara nchini Jordan kwa mazungumzo juu ya kutuliza mzozo katika kanda ya Mashariki ya Kati. Waziri Maas anataka ufafanuzi kuhusu hatma ya wanajeshi wake Iraq.

Waziri Heiko Maas amesema ni katika maslahi ya kila mmoja kuendeleza mapambano dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, kama sehemu ya muungano wa kimataifa nchini Iraq, ili kulinda mafanikio yaliofikiwa huko awali.

“Ni muhimu kwamba sisi kama washirika wa muungano dhidi ya IS tunaendelea kuwepo nchini Iraq na ni muhimu pia kwa Iraq na tunafanya mazungumzo na serikali kuhusu umuhimu wa kubakia kwa vikosi vya kimataifa licha ya uamuzi wa bunge kutaka vikosi hivyo viondoke,” alisema Maas na kuongeza kuwa “tunahofia kwamba iwapo vikosi vya kimataifa vitaondoka kitisho cha IS kitarejea kuwa kikubwa.”

Heiko Maas alitoa matamshi hayo katika mkutano wa waandishi habari aliouhutubia pamoja na mwenzake wa Jordan Ayman Al Safadi katika mji mkuu wa Amman.

Ujerumani iliwahamisha wanajeshi wake 35 wanaohudumu nchini Iraq katika mataifa jirani ya Jordan na Kuwait siku ya Jumanne, kufuatia tafrani iliyosababishwa na kitendo cha Marekani kumuuwa Jenerali wa Iran katika shambulio la ndege mjini Baghdad wiki iliyopita.

(Visited 27 times, 1 visits today)
Share this post