ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU TAREHE 20-01-2020

2811
0
Share:

Everton inajiandaa kuwasilisha dau la £30m kumnunua kiungo wa kati wa Juventus Mjerumani Emre Can, ambaye mkataba wa sasa umekamilika. (Sunday Mirror)Liverpool itamenyana na Chelsea kumsaka mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner,23. (Sunday Mirror)Mkurugenzi wa Lille Luis Campos huenda akjijiunga Manchester United katika wadhifa sawa na huo. (Sun on Sunday)Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel, amesema klabu hiyo bado inamhitaji beki Layvin Kurzawa. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 27-ananyatiwa na Arsenal.(Goal)Manchester City wanajiandaa kupokea ofa ya PSG ya kumnunua Pep Guardiola, ikiwa klabu hiyo inayo ya Ligue 1 itamtimua Tuchel. (Sunday Express)

Layvin Kurzawa

Manchester United imeshindwa na Real Madrid katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, 22. (Daily Star Sunday)Mkurugenzi wa kiufundi wa Arsenal, Edu amekutana na wawakilishi wa kiungo wa kati ma mlizi wa Athletico Paranaense, Bruno Guimaraes kuhusiana na uwezekano wa kununua kwa kiasi hadi cha euro milioni 30 sawa na (£25.6m) kumpata mchezaji huyo wa Brazili wa miaka 22. (Goal – in Portuguese)PSG iko tayari kumpatia ofa ya mkataba wa thamani ya euro milioni 12 kwa mwaka, kiungo wa kimataifa wa Senegal Kalidou Koulibaly, 28, akikubali kuondoka Napoli. (Foot Mercato – in French)

Senegal Kalidou Koulibaly

Klabu ya Roma ya Italia inataka kumsaini winga wa zamani wa Manchester United Adnan Januzaj kwa mkopo kutoka Real Sociedad, kwa lengo la kumnunua kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji msimu wa joto. (Mail on Sunday)Mkufunzi wa Tottenham Hotspur boss Jose Mourinho ana matumaini ya kumsajili mshambuliaji mwezi huu wa Januari, baada ya kukosa huduma ya Harry Kane ambaye anauguza jeraha kwa hadi miezi mitatu. (Evening Standard)Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, ataomba Paris St-Germain isimshirikishe katika mechi ya Jumapili dhidi ya Lorient ili kushinikiza uhamisho wa kwenda Atletico Madrid. (Marca)

Edinson Cavani

Newcastle United wanakaribia kumsaini kwa mkopo winga wa Austria Valentino Lazaro, 23, kutoka Inter Milan, wakitarajia kumnunua kwa 20m euro (£17m). (Tuttomercatoweb – in Italian)Real Madrid imepuuzilia mbali ofa ya kutaka kumsajili kwa mkopo James Rodriguez,28, na wako tayari kumuuza kiungo huyo wa kati wa kimataifa wa Colombia. (Marca)Atletico huenda ikamnunua Alexandre Lacazette, 28, wa Arsenal au Paco Alcacer, 26, wa Borussia Dortmund ikishindwa kumsajili Cavani. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Alexandre Lacazette

Juventus imewasilisha ofa ya kumuuza kiungo wa kati wa Italia Federico Bernardeschi, 25, kwa Barcelona kama sehemu ya makubaliano ya kumpata kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 31. (AS)Kiungo wa kati wa Flamengo Reinier Jesus, 17, amekutana na wawakilishi wa Real Madrid kukamilisha mpango wa uhamisho wake. (AS)Mkufunzi wa Aston Villa Dean Smith, amesdokeza kuwa klabu hiyo inakaribia inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Genk na Tanzania Mbwana Samatta, 27. (Birmingham Mail)

Mbwana Samatta
(Visited 1,336 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us