ASSAs

DALILI SABA ZA KUMGUNDUA MPENZI WAKO KAMA ANAKUSALITI

1175
0
Share:

1. MABADILIKO YA TABIA.
Katika kuishi pamoja kimahusiano, bila shaka mtakuwa mmekwishasomana tabia kwa kiwango cha kutosha; utajua ratiba ya mwenzi wako, mitoko yake, marafiki zake, namna ya mawasiliano, nk. Sasa inapotokea mambo yakabadilika; alikuwa anarudi nyumbani mapema baada ya kutoka kazini, lakini ghafla tu anaanza kuchelewa bila sababu za msingi; ulikuwa unajua password za simu yake, lakini ghafla amebadili na hataki kukupatia. Ulikuwa unajua maeneo anayopenda kufanyia mitoko yake, lakini mara tu unagundua amehamishia mitoko yake sehemu mpya na hajakwambia, nk. Kasumba za usiri kama hizo zikianza kushamiri, ni ishara dhahiri kwamba, ndani ya mahusiano yenu, uaminifu umeanza kuadimika.

2. MABADILIKO YA FURAHA YASIYO TABIRIKA.
Katika mahusiano, hutokezea hali za sintofahamu za hapa na pale ambazo, hutatulika mapema. Lakini, ghafla tu mwenziyo analazimisha sintofahamu hizo zikuze ugomvi ambao utawafanya msionane au msiwasiliane siku nzima. Kimsingi, hapo utamwona mwenzi akitafuta mazingira ya kujiweka mbali nawe ili kuwa huru kufanya mambo yake bila bughudha. Ikifikia hali hiyo, bila shaka kidudumtu kimeshaingilia mahusiano yenu. Chukua hatua.

3. ZAWADI ZA GHAFLA AU ZISIZOZOELEKA.
Kupeana zawadi mara kwa mara, ni jambo zuri na linachipulisha huba. Lakini pamoja na hayo, inapotokea mwenzi wako ambaye, hakuwa na desturi ya kukuletea zawadi mara kwa mara, ghafla tu hata kama si birthday wala kumbukumbu nyingine yoyote, akaanza tu kukushitukiza na zawadi zisizitabirika, anza kumchunguza. Watafiti wa tabia za mwanaadamu wamekubaliana kwamba, mtu anapotenda uovu (usaliti) hujishitukia sana, na kutafuta namna ya kufidia uovu huo kwa mwenzi. Kufikia hapo, zawadi za ghafla zinaweza kutumika kama fidia kwako.

4. KUKITHIRI KWA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII.
Siku hizi, wasaliti wengi hutumia zaidi mitandao ya kijamii kuwasiliana, kukutana na kuratibu miadi na wapenzi wao wapya. Hivyo, unapoona mwenzi wako ambaye, hana sababu za msingi za kumuweka mitandaoni muda mwingi, lakini ghafla tu amekuwa busy kuchat mitandaoni kiasi cha kuathiri shughuli nyinginezo, chukua hatua mapema, hiyo ni kengere ya hatari dhidi ya mahusiano yenu.

5. KUKOSA MUDA NA WEWE
Unapoona uko kwenye mahusiano na mtu ambaye, muda wote akiwa mbali na wewe hataabiki kukutafuta japo kukujulia hali, na hata anapokuwa karibu nawe, anakuwa busy na simu, mitandao, au na jambo lingine, hiyo ni ishara mbaya. Mara nyingi, usaliti unapoingia ndani, mwenzi hukosa uwezo wa kudhibi muda na hisia zake baina yako na penzi lake jipya.

6. KUJIBADILI MWONEKANO NA MATENDO YA NJE.
Unapoona mpenzi wako ameanza kujibiisha kuboresha mwonekano wake anapotoka nje, anza kumchunguza. Siku zote mtu anapooanza kujihusisha na mahusiano mapya, hujitahidi kujipendezesha; kama alikuwa hapigi pasi nguo, sasa utashangaa anapiga pasi mpaka soksi; kama alikuwa hajipulizi marashi, sasa utashangaa ananunua marashi ya namna zaidi hata ya tatu; kama mswaki alikuwa anapiga bila dawa, ghafla utamwona amekuja na kubwa; kama nywele alikuwa akinyoa kwa mwezi mara moja, sasa utashangaa kuona kila wiki akiingia Saloon. Yote hayo, anayafanya anapotaka kutoka, lakini anapokuwa nyumbani anakuwa kawaida tu, si katika umaridadi ule anapotaka kwenda mbali nawe.

7. KUKUEPUSHA NA SIMU YAKE.
Mahusiano yenye afya hujengwa na uaminifu. Kama mnaaminiana, na hamsalitiani, hakuna sababu ya kufichiana simu wala password. Kwa hivi, unapoanza kuona mwenzi anadhibiti sana mawasiliano yake; hataki kukuachia simu, na hata akikuachia anakuwa juujuu kutaka kujua unachofanya, hiyo ni dalili kubwa ya kukosekana uaminifu.

(Visited 441 times, 1 visits today)
Share this post