ASSAs

KAULI YA ADO SHAIBU BAADA YA LOWASA, SUMAYE KURUDI CCM

712
0
Share:

Vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa makini na kuwachuja wanasiasa wanaotoka chama cha mapinduzi CCM  hasa wale waliowahi kuwa na madaraka na kushiriki kuwahujumu wapinzani, kuwafunga na kuwaminya kwakuwa awawezi kubadilika na kuwa wazuri kwa wapinzani.

 Kauli hiyo imetolewa leo na   Katibu wa Uenezi wa Chama hicho Ado Shaibu alipofanyiwa mahojiano na muungwana blog na kusema kuwa mtu kama Lowasa na Sumaye wameshachoka maisha ya kisiasa wameamua wachukue mkondo tu wakufanya  maisha yao binafsi.

“Hama hama za wanasiasa kurudi kwenye chama cha CCM ni ishara ya kigeu geu na unafki sumaye alipoingia Chadema alijenga hoja ya kwamba aliona ndani ya CCM hakuna demokrasia na kuamua kujiunga CHADEMA ili kuujenga  upinzani utakaokuja kuiondoa CCM madarakani’ alisema Ado Shaibu.

“Sumaye alijenga hoja kuwa hata apewe trilioni 50 awezi kurudi CCM na alieleza kuwa aliweza kupitia misukosuko mingi ndani ya biashara zake na maisha yake, sasa anarudi CCM na kusema CCM ni nyumbani inaonyesha mwanasiasa kigeugeu” alisema Ado

Ado alisema ilo liwe funzo  kwa wapinzani kwa wanaotoka CCM kwenda upinzani wanatakiwa kumulikwa kwa umakini kwakuwa lipo kundi la kwanza la wana CCM ni kweli wapiganaji wamekosa haki wanakuja upinzani kuidai haki hiyo kwenye mageuzi, hao wakaribishwe.

(Visited 108 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us