ASSAs

WAZIRI KIGWANGALLA AWAOMBEA MSAMAHA WALIOSAMBAZA PICHA ZA UHARIBIFU BARABARA NGORONGORO

393
0
Share:

Waongoza utalii ambao walisambaza video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha uharibifu wa barabara kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wameombewa msamaha na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk Hamis Kigwangalla

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Dk Kigwangalla ameandika kuwa amemuomba Mkuu wa mkoa wa Arusha Nchini Tanzania, Mrisho Gambo na kamati ya ulinzi kuwasamehe na kuchukulia hilo kama onyo.

Kigwangalla amesema kwa kuwa ni tukio la kwanza, amempongeza Gambo kuingilia kati suala hilo ambalo ameeleza linalinda hadhi ya nchi.

“Hivi tour guide anayetangaza kwamba Ngorongoro hakupitiki anapata faida gani? kama wageni wakiacha kuja Waziri nanyimwa mshahara ama posho zangu? Ama ni yeye atakayekosa biashara? Watanzania tukae kimkakati jamani,” ameandika.

Amesema ni vema taarifa kama hizo wawe wanazifikisha mahala husika ili zipatiwe ufumbuzi na ikishindikana afikishiwe Waziri moja kwa moja.

(Visited 48 times, 1 visits today)
Share this post