ASSAs

MISS RWANDA APATIKANA, KULIPWA MSHAHARA KILA MWEZI

649
0
Share:

Safari ya kuelekea kushiriki Miss World 2020 imekamilika Rwanda baada ya kumpata mwakilishi wao, Naomie Nishimwe aliyetwaa taji la Miss Rwanda na kumpa zawadi ya gari ambapo atakua atalipwa mshahara wa kila mwezi.

Naomie alitwaa taji la Miss Rwanda, katika fainali zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa mikutano wa Intare Arena nchini humo.

Mrembo huyo ambaye alishiriki katika Miss Kigali, alichuana na warembo wengine 19 ambapo mbali ya kuwa Miss Rwanda pia alishinda kipengele cha Miss Photogenic.

Naomie ataiwakilisha Rwanda katika Miss World, shindano linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu nchini Thailand.

Kutokana na ushindi huo Naomie alipata zawadi mbalimbali ikiwemo gari aina ya Suzuki Swift lenye thamani ya Sh43 milioni.

(Visited 93 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us