ASSAs

DIAMOND AWASILI STUDIO ZA SWIZZ BEATZ MAREKANI

901
0
Share:

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, ameonekana akiwa katika studio za mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz.
Hilo linatokea ikiwa ni siku chache zimepita tangu mtayarishaji huyo, aweke wimbo wa ‘Gere’ ulioimbwa na Tanasha Donna akimshirikisha Diamond na ile ya singeli ya ‘Wanga’ iliyoimbwa na Meja Kunta akimshirikisha Lavalava wa lebo ya WCB katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.
Kama haitoshi siku sita zilizopita mtayarishaji huyo aliweka video katika ukurasa wake ikimuonyesha  mwanamuziki Alicia Keys ambaye ni mke wake akionekana kucheza wimbo wa Wanga.

Katika picha hiyo, Diamond ameandika ’Kanda! Kanda! nipo na mfalme ananifanya nijisikie kama nipo nyumbani Tanzania, najisikia kama  LasAngelos  ni nyumbani kwangu pa pili”.

(Visited 145 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us