ASSAs

BILLY GILMOUR MWAROBAINI WA LIVERPOOL FA CUP

1378
0
Share:

Nilipo sikia kuhusu Ugonjwa wa Corona nilihisi tu pengine ni laana za Wachina huko Uchinani, nilihisi pengine ni zile laana za wao kula wadudu na wanyama ambao hata mimi na wewe hatuwezi hata kuwasogelea. Corona ikaanza kuwa tishio nchini China.

Sikutaka tena kuendelea kufuatilia kesi hiyo, nikaiacha iende zake huko. Kwa sasa Corona ni ugonjwa hatari Dunia, ikiripotiwa kuingia hadi nchi tano za Afrika kama SENEGAL na MOROCCO. Huu ugonjwa ni tishio sana kwa sasa. Niliposikia ugonjwa huu umeingia Afrika huku viongozi wakisisitiza haturuhusiwi kusalimiana kwa kushikana mikono wala kapigana mabusu, niliamuwa kujifungia ndani nikawasha runinga yangu.

Mchezo ulio wakutanisha Chelsea dhidi ya Liverpool ulinifanya nitulie na kusahau kabisa kuhusu Corona, macho yangu yalikuwa miguuni mwa kijana mmoja ambaye alinifanya nikumbuke zama za wafalme pale Chelsea. Nilikuwa nikimtazama bwana mdogo aliyeitwa Billy Gilmour mwenye umri wa miaka 18 tu.

Achilia Mbali ufundi ulio jaa kwenye miguu yake bali kiungo huyu alikuwa chini ya ulinzi mkali wa askari walio tukuka wa Jurgen Klopp ambao ni Fabinho, Adam Lallana na James Millner, Sasa wacha nikupe simulizi tamu ya Bwana mdogo huyu.

June 11, 2011 huko nchini Scotland katika viunga vya Glasgow alizaliwa Bwana mdogo huyu, Baba Yake aliyeitwa Clifford alimpa jina la Billy, Bwana mdogo huyu ana sifa inayo mtofautisha na wengine ndiyo maana nika aanda makala hii fupi ili umfahamu vizuri Billy Gilmour.

Mara ya kwanza Mashabiki wa Chelsea walimuona Gilmour kwenye mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Manchester United, lakini Bwana mdogo huyu alianza kuonyesha maajabu Yake kwenye klabu ya Rangers chini ya miaka 20 lakini wakati huo Gilmour alikuwa na miada 15 tu, uwezo wake ulimfanya Gilmour ajumuishwe kwenye kikosi cha vijana wenye miaka 20 lakini pia kwa wakati huo huo aliitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Scotland chini ya miaka 21, Alipo jiunga Chelsea alianza kucheza kwenye kikosi cha Chelsea umri chini ya miaka 23.

jambo jingine embalo hulijui kuhusu Bwana modo huyu ni kwamba anacheza nafasi nyingi uwanjani ikiwemo kiungo mkabaji, kiungo mshambuliaji, ana kaba na kushambulia kwa wakati mmoja (Box to Box Midfield).

Hebu turudi kwenye mchezo wa FA Cup, Chelsea ina pata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Liverpool ambayo imepoteza michezo mitatu mfululizo huku ikishindwa kufunga goli hata moja na ikiruhusu wavu wao kuguswa mara saba. Ushindi huu wa Flank Lampard haukuja kama ngekewa bali ni mbinu ya kuamuwa mchezo, namna alivyo kuwa imara katikati ya uwanja, namna alivyo wapa majukumu viungo wake akiwemo Gilmour ambaye alizungukwa na Kovasic na Ross Barkley ambao kazi yao ilikuwa ni kukimbia kuelekea mbele huku kazi ya kukaba ikifanywa na Bwana mdogo Billy Gilmour. Bwana mdogo huyu aliwapa wakati mgumu Fabinho na Lallana ambao walikuwa wana shindwa kupandisha mashambulizi kuelekea langoni kwa Chelsea, Gilmour aliifanya Chelsea kuwa salama zaidi.

Anachotakiwa kwa sasa Frank ni kumpa muda kijana huyu kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea pindi Ng’olo Kante anapo kosekana, Gilmour ni zaidi ya kiungo, miaka michache ijayo Chelsea watakuwa wameokoa kiasi kikubwa cha fedha kupitia kwa kiungo huyu Billy Gilmour.

(Visited 253 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us