ASSAs

CHADEMA KUVAA NGUO NYEUPE

935
0
Share:

Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kanda ya Pwani kimewataka wanachama wake kuvaa nguo nyeupe au kufunga kitambaa cheupe kuanzia leo Machi 7, 2020 kama ishara ya kutaka haki itendeke katika kesi ya viongozi wa chama hicho machi 10 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na katibu wa kanda hiyo Hemed Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari ametoa wito kwa wananchama wote kufanya hivyo.

Katika mashtaka 13 yanayowakabili viongozi wanne wa Chama hicho pamoja na katibu mkuu wa zamani wa Chadema  Dkt. Mashinji yakiwemo ya kufanya mikusanyiko kinyume cha sheria na kusababisha woga na hofu kwa wakazi wa kinondoni na kifo cha Akwelina Akwilina.

Viongozi hao ni mwenyekiti wa Chdema Freeman  Mbowe, katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika ambapo siku ya jana viongozi wa Wakuu na wabunge wa Chadema walifunga kazi baada ya kuwasilisha hoja zao za majumuisho katika kesi ya jinai inayowakabili katika mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu.

(Visited 132 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us