ASSAs

KESI INAYOMKABILI KIGOGO WA CCM YAPIGWA KALENDA

1032
0
Share:

kesi ya jinai inayomkabili mfanyabiashara ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UWT-CCM Wilaya ya Kinondoni, Frolence Masunga (45) mkazi wa Kimara Suka jijini Dar es Salaam imeahirishwa tena.

Kesi hiyo imetajwa kwa mara ya pili leo Machi 9,2020 ambapo ilishatajwa kwa mara ya kwanza Januari 22,2020 katika mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, inayoendeshwa na Hakimu mfawidhi Martha Mpanze.

Masunga anashtakiwa kwa Kosa la kuchukua Fedha za Abdallah Majora Bulembo, kwa njia ya udanganyifu.

Imeelezwa kuwa mnamo Disemba,2019 katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam Masunga alipokea kiasi cha fedha za kitanzania millioni 100 kutoka kwa Bulembo kwa lengo la kumuuzia nyumba iliyopo Kinyerezi ndani ya manispaa ya ilala, ambapo baadae hakuweza kukabidhi nyaraka za nyumba hiyo kwa Bulembo hivyo nyumba hiyo kuendelea kubaki mikononi mwake.

kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Martha Mpanze imeahirishwa ambapo imetajwa kusikilizwa tena machi 25/2020 mahakamani hapo.

(Visited 273 times, 1 visits today)
Share this post