ASSAs

KOCHA WA ARSENAL MIKEL ARTETA AKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA

357
0
Share:

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekutwa na virusi vya ugonjwa wa corona na mechi kati ya timu yake na Brighton iliyotarajiwa kuchezwa wikiendi imeahirishwa.

The Gunners wamefunga uwanja wao wa mazoezi na wafanyakazi waklabu hiyo ambao waligusana na Arteta wamelazimika kujiweka karantini.

Ligi ya Premier itafanya mkutano wa dharura na klabu zote siku ya Ijumaa ili kuzungumzia kuhusu mechi zinazotarajiwa kuchezwa.

”Hii kwa kweli inasikitisha” , alisema raia wa Uhispania Arteta mwenye umri wa miaka 37.

”Niliamua kupimwa baada ya kujihisi vibaya lakini nitarudi kazini mara tu nitakaporuhusiwa kufanya hivyo”.

”Wachezaji wote wa Chelsea waliogusana naye kikiwemo kikosi chote cha wachezaji 11, wafanyakazi pamoja na wakufunzi sasa watahitajika kujiweka karantini kwa kipindi cha siku 14” , ilisema klabu hiyo ya ligi ya Premia.

Licha ya kupatikana na ugonjwa huo callum anaendelea vyema na anatarajia kurudi katika uwanja wa mazoezi atakaporuhusiwa, ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Arsenal inatarajia kwamba idadi kubwa ya wafanyakazi na kikosi chote cha kwanza kitalazimika kujiweka karantini.

Klabu hiyo ilikuwa ikitarajiwa kukabiliana na Brighton katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi mwendo wa saa 11 jioni lakini Brighton ikatoa taarifa muda mfupi baada ya Arteta kugunduliwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ikitangaza kwamba mechi hiyo imeahirishwa.

BBC Sport inaelewa kwamba vilabu vyote vya ligi ya England vinataka kuamua kuhusu uamuzi wa pamoja na mojawapo ya uamuzi huo ambao utajadiliwa katika mkutano ni kuahirisha mechi zote zitakazochezwa wikiendi hii.

”Afya ya watu wetu na umma kwa jumla ni jukumu letu na hapo ndipo tunapoangazia kwa sasa” ,alisema mkurugenzi mkuu wa Arsenal Vinai Venkatesham.

”Tunaendelea na mazungumzo kwa wote wanaoshukiwa kupata maambukizi ili kukabiliana na hali vizuri, na tunatarajia kurudi katika mazoezi hivi karibuni pindi tu ushauri wa kiafya utakapoturuhusu”.

Mechi ya ligi ya Uingereza kati ya Arsenal na Manchster City pia imeahirishwa siku ya Jumatano kama hatua ya tahadhari kabla ya wachezaji kadhaa wa Arsenal kujiweka katika karantini baada ya mmiliki wa Olympiakos Evangelos Marinakis kuambukizwa virusi hivyo.

Arsenal ilisema kwamba Marinakis , 52 alikutana na wachezaji wake kadhaa wakati Arsenal ilipocheza mechi ya kombe la Yuropa dhidi ya Olympiakos katika uwanja wa Emirates wiki mbili zilizopita.

Klabu hiyo ilisema kwamba hakuna mfanyakazi ama mchezaji atakayefanyiwa vipimo vya virusi vya corona.

Wakati huohuo beki wa Manchester City Benjamin Mendy amejiweka katika karantini kama hatua za tahadhari baada ya nduguye mmoja kulazwa hospitalini akionesha dalili za ugonjwa wa corona.

(Visited 32 times, 1 visits today)
Share this post