ASSAs

KISA CORONA, LADY GAGA AFANYA MAAMUZI HAYA KUHUSU ALBUM YAKE

788
0
Share:

Lady Gaga Siku ya Jumanne alitangaza kwamba baada ya “kufikiria sana,” ameamua kuahirisha kuiachia album yake kufutia mlipuko wa Corona

“Huu ni wakati mgumu na wa kutisha kwa sisi sote, Japo ninaamini sanaa ni moja wapo ya vitu vyenye nguvu ya kuleta furaha na uponyaji wakati wa nyakati kama hizi, haijakaa sawa kwangu kutoa hii albamu na haya yote yanayoendelea ulimwengu wakati wa hili janga “aliandika kwenye barua ya wazi aliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii

LadyGaga amesema kuwa atatangaza tarehe mpya ya kuiachaia Album hiyo ambayo ilikuwa imepangwa kutoka April 10, Ameweka wazi pia kuwa alikuwa amepanga kuwa-suprise mashabiki kwa kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella ambalo pia limetangazwa kufanyika mwezi wa Kumi mwaka huu kupunguza maambukizi ya virusi vya corona

(Visited 75 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us