ASSAs

CORONA: WASIO NA AJIRA WAONGEZEKA MAREKANI

480
0
Share:

Kufungwa kwa shughuli za kiuchumi kutokana na janga la virusi vya corona Marekani kumesababisha ongezeko kubwa la wanaosajiliwa kwenye orodha ya wasio na ajira, na kufika Watu Milioni 3.3, idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini humo. •

Ripoti ya wasio na ajira ambayo ni utaratibu wa kawaida Marekani, imeongezeka kipindi hiki baada kufungwa kwa migahawa, maduka, hoteli na biashara nyingine. •

Karibu kila jimbo la Marekani limesema corona ndio sababu kuu ya kuongezeka kwa idadi ya wasio na kazi,kunakokwenda sambamba na athari hasi katika sekta za chakula, hoteli, burudani, afya na usafiri, lakini Trump anasema ana imani ajira zitapanda kwa kasi hivi karibuni.

(Visited 39 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us