ASSAs

KENYA: WATAKAOKUTWA NJE KUANZIA SAA 1 JIONI-11 ASUBUHI KUKAMATWA

908
0
Share:

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Hillary Mutyambai ameonya kuwa watu wote watakaokutwa nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja asubuhi watawajibishwa kwa mujibu wa Sheria

Onyo hilo linakuja siku chache baada ya Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kutoa amri ya watu kutotoka nje katika muda huo ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo

IGP Mutyambi amesema mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo atakamatwa na kufungulia kesi Mahakamani. Watakaoruhusiwa kutoka ni watoa huduma muhimu na wanatakiwa kuwa na vitambulisho

Amewataka Wakenya kubaki nyumbani ili kuepuka adha hiyo kwakuwa Polisi nchi nzima watakuwa kazini kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa

(Visited 182 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us