ASSAs

WHO YASEMA KUNA UPUNGUFU WA WAUGUZI MILIONI SITA DUNIANI

669
0
Share:

Shirika la afya duniani WHO limesema kuna upungufu wa wauguzi milioni sita duniani.

Shirika hilo limesema katika ripoti yake kwamba upungufu huo upo hasa kwenye sehemu masikini, ikiwa pamoja na barani Afrika, kusini mashariki mwa bara Asia na Amerika ya kusini.

 Shirika la WHO limeeleza kwamba wauguzi ndio nguzo ya kila mfumo wa afya na limetilia maanani kwamba manesi ndiyo kwa sasa wamesimama mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Mkurugenzi wa asasi hiyo Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito wa kuwapa wahudumu hao wa afya kila msaada wanaohitaji.

(Visited 62 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us