ASSAs

MAKUBALIANO YA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAFUTA YAFIKIA HAPA

955
0
Share:

Wazalishaji na washirika wa nchi zinazouza mafuta wamekubaliana kufikia makubaliano na kupunguza uzalishaji kote duniani kwa takribani asilimia 10 baada ya hitaji kupungua pakubwa kwasababu ya amri ya kusalia majumbani kama njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa Jumapili kupitia mkutano uliofanyika kwa njia ya video, ni ya kwanza kupunguza uzalishaji mkubwa wa mafuta ambayo hayajawahi kufikiwa siku za nyuma.

Shirika la nchi zinazozalisha mafuta (OPEC) na washirika wake ikiwemo Urusi, lilitangaza mipango ya kufikia makubaliano hayo Aprili 9 ingawa Mexico haikuridhia ombi hilo.

Opec bado haijatangaza rasmi makubaliano hayo lakini nchi husika zimethibitisha kuwa ziko tayari kwa mabadiliko.

Kile kilichothibititshwa hadi kufikia sasa, ni kwamba wazalishaji hao na washirika wake watapunguza uzalishaji wa mapipa milioni 9.7 kwa siku.

Jumatatu, Barani Asia bei ya mafuta ilipanda kwa zaidi ya dola 1 kwa pipa na kiwango cha mafuta ghafi cha asilimia 3.9 yakiuzwa kwa dola 32.71 kwa pipa huku Marekani asilimia 6.1 ikiuzwa kwa dola 24.15 kwa pipa.

Hisa nchini Australia zilipanda kutoka asilimia 3.46 zikiongozwa na wauzaji wa mafuta lakini nchini Japani hisa za Nikkei 225 zilishuka kwa asilimia 1.35 kwasababu ya wasiwasi wa hitaji lililoshuka duniani kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona.

“Makubaliano haya hayajawahi kufikiwa kabla kwasababu sio tu kati ya wazalishaji wa Opec na washirika wake… lakini pia na wauzaji wakubwa duniani ambao ni Marekani pamoja na nchi zingine za G-20 ambazo zimekubali kuunga mkono makubaliano hayo kwa kupunguza uzalishaji,” Sandy Fielden, mkurugenzi wa utafiti wa mafuta katika kampuni ya Morningstar, ameiambia BBC.

Rais wa Marekani Donald Trump na waziri wa nishati wa Kuwait Daktari Khaled Ali Mohammed al-Fadhel waliandika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, huku waziri wa kawi wa Saudi Arabia na Shirika la habari la Urusi linalomilikiwa na serikali (TASS) wakithibitisha makubaliano hayo Jumapili.

“Kwa uwezo wa Mungu na ungozi wa busara, juhudi na mazungumzo endelevu tangu alfajiri Ijumaa, sasa tunatangaza kufikiwa kwa makubaliano ya kihistoria ya kupunguza uzalishaji kwa takriban mapipa milioni 10 ya mafuta kutoka kwa nchi za wazalishaji wa mafuta OPEC kuanzia Mei Mosi, 2020,” ameandika Dr al-Fadhel kwenye mtandao wa Twitter.

(Visited 159 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us