ASSAs

WAGONJWA WA CORONA TANZANIA WAFIKIA 147

491
0
Share:

IDADI ya kesi za wagonjwa wa Covid 19 nchini Tanzania imeongezeka na kufikia kesi 147, baada ya wagonjwa wengine wapya 53 kukutwa na virusi vya Corona.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema wagonjwa hao wote ni Watanzania ambapo 38 ni kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Zanzibar wagonjwa 10, Kilimanjaro mgonjwa mmoja, Mwanza mgonjwa mmoja, Pwani mgonjwa mmoja, Lindi mgonjwa mmoja na Kagera mgonjwa mmoja.

(Visited 57 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us