ASSAs

UJUMBE WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KUTOKA KWA RAIS WA UTURUKI

743
0
Share:

Rais wa Uturuki  na  msemaji wa Bunge  wawatakia waislamu wote funga na ibada njema za Mwezi Mtukufu wa Rmadhani.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan na msemaji wa bunge la taifa wawatakia waislamu wote ulimwenguni funga njema ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na ibada njema  za mwezi huo mtukufu katika  kalenda ya kiislamu.

Rais Erdoğan ameandika katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe kuhusu  kuingia kwa Mwezi Mtukufu wa Rmadhani na kuukaribisha kwa imani kama ilivyoagizwa na Mtume.

Katika ujumbe wake wa Twitter ulioambatanishwa na picha ya Al Kaaba na maneno yanayopatikana katika Quran Sura ya Pili Aya ya  183, aya ambayo inawakumbusha waislamu : “Enye waislamu, mmefaradhishiwa kufunga katika  Mwezi  Mtukufu wa Rmadhani kama walivyofaradhishiwa wakabla yenu ili muweze kuwa wachamungu”.

Msemaji wa Bunge la Uturuki Mustafa Sentop nae pia amewatakia waislamu mwanzo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kuwakumbusha kuendelea kuheshi maagizo yaliotolewa katika juhudi za kupambana na  virusi vya corona na kujikinga na maambukizi.

(Visited 85 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us