ASSAs

NIYONZIMA ATAJA WACHEZAJI WAKE BORA TANZANIA ALIOWAHI KUCHEZA NAO

909
0
Share:

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima leo alikuwa mahojiano na kituo cha Radio cha East Afrika na kufunguka mambo mbalimbali kuhusiana na soka.

Wakati wa mahojiano hayo Haruna Niyonzima aliulizwa kuhusiana na anazungumziaje uwezo wa Yikpe ambao amekuwa akiuonesha akiwa Yanga na kukataa kujibu swali hilo ila amejibu kuhusiana na mchezaji wake bora aliyewahi kucheza nae Tanzani toka aingie nchini.

”Mchezaji wangu bora kwanza nataja wawili kuna Kelvin Yondani sio kwamba ni rafiki yangu lakini ni mchezaji mzuri pia Erasto Nyoni nina wachezaji wengi tu ambao sijawataja sio kwamba sio wazuri lakini nimechukua hao wawili wananikosha” alisema Niyonzima

Haruna Niyonzima amecheza soka Tanzania toka 2011 alipojiunga na Yanga akitokea APR ya kwao Rwanda hadi 2017 akajiunga na Simba SC (2017-2019) na sasa amerejea tena Yanga SC 2020 na kuendelea kufanya vizuri.

(Visited 421 times, 1 visits today)
Share this post