ASSAs

KIKAO CHA BUNGE CHAVURUGWA KWA PICHA ZA NGONO AFRIKA KUSINI

838
0
Share:

Mkutano wa kamati ya bunge kwa njia ya mtandao Afrika Kusini umevamiwa na wadukuzi na spika kudhalilishwa.

Kikao hicho kilikuwa tu ndio kimeanza Alhamisi asubuhi wakati ambapo picha za ngono zilipojitokeza kwenye skrini huku sauti ya mwanamume ikisikika kumtusi Spika Thandi Modise, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.

Spika huyo aliyeshikwa na hasira alipaza sauti akisema hiyo ndio sababu anapinga mikutano ya mitandaoni. “Hiki kilichotokea ni kilekile nilichokuwa ninakisema kuhusu kufanya mikutano kwa njia ya Zoom!” Bi Modise amenukuliwa akisema hivyo na tovuti ya Times Live.

Wabunge walielezea tukio hilo kama lenye kukera na kutatiza akili, kulingana na Tovuti ya habari ya Eyewitness.
Iliwalazimu wahandisi wa Bunge kutuma kiunganishi chengine ambapo wabunge waliunganika tena na kuendelea na kikao chao.

(Visited 134 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us