ASSAs

POLISI: MASOUD AMEFIA HOTELINI

1519
0
Share:

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Ukerewe (OCCID), Masoud Mohammed amekutwa amefariki ghafla Hotelini, Masoud ni mmoja wa Maaskari waliobadilishwa vituo hivi karibuni kutoka Bunda, Mara na kupelekwa Ukerewe, Mwanza.

Masoud ndio kwanza alikuwa amepandishwa cheo na kuwa OCCID na kituo chake cha kwanza cha kufanya kazi kama OCCID ilikuwa ni hapo Ukerewe.

RPC Mwanza amesema Masoud alipofika Ukerewe kuanza kazi ya OCCID alikosa nyumba hivyo alikuwa anaishi Hotelini, asubuhi ya leo walishangaa kuona haamki, walipovunja mlango akakutwa amefariki.

Hivi karibuni Masoud Mohammed alijizolea umaarufu baada ya video zake kusambaa mitandaoni akisoma Qur’an Tukufu .

(Visited 943 times, 1 visits today)
Share this post