ASSAs

MEMBE: TUTATENGWA NA MAJIRANI WAKIONA HATUFUATI VIGEZO VYA WHO KUPAMBANA NA CORONA

740
0
Share:

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amezungumzia uhusiano wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na nchi za jirani katika kipindi hiki cha mlipuko wa Corona

Amesema, kwasasa nchi zipo katika mapambanao dhidi ya Corona ndio maana nchi kama Zambia zinafunga mipaka yake na kuzuia watu waziende ikiwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo kutoka sehemu moja

Aidha, kuhusu kupimwa kwa Madereva wa Tanzania wanaotaka kuingia Kenya, amesema Kidiplomasia ni kwamba nchi za jirani zina wasiwasi sana kwamba Tanzania inaweza kuwa inapeleka ugonjwa huu kwenye nchi fulani

Ameeleza “Wasiwasi huu unaweza kuwa unakuja baada ya kuona pengine hatufungamani ni vigezo vya WHO ambavyo vimewekwa na dunia nzima vinavifuata labda mpaka pale tutakapofungamana na vigezo vya WHO wanavyofuata wenzetu”

Ameongeza “Kwa namna Tanzania inavyoshungulikia janga kama hili tutatengwa, majirani watatutenga na kutengwa ni kwa namna hii ya kufunga mipaka na kidiplomasia tunasema mtengano huu unatuumiza na kututesa zaidi sisi kuliko majirani”

Amemalizia kuwa ni kweli diplomasia imeshuka kwasababu awamu hii haijengi kwenda na dunia inaangalia zaidi matatizo ya ndani na ina athari zake hasa tukipata janga kama hili na ndio maana tunasema diplomasia imeshuka sana

(Visited 184 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us