ASSAs

LEWANDOWSKI ATAJA NAMBA 9 ZAKE HATARI DUNIANI

1260
0
Share:

Dunia ya soka inamtambua kuwa ni moja ya washambuliaji bora kuwahi kutokea, ni Robert Lewandowski anayekipiga Bayern Munich. Lakini pia na yeye anao washambuliaji wake ambao anaamini ni bora.

Lewandowski akifanyiwa mahojiano na gazeti la Bild la Ujerumani, aliambiwa ataje namba 9 zake bora duniani.

Lakini katika swali hilo Lewy hakutakiwa kujijumulisha yeye mwenyewe katika orodha, ambapo aliwaacha Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao wao hawahesabiki kama namba 9 za asili.

“Hilo si swali rahisi,” Lewandowski aliiambia Bild.

“Kama tunaongelea washambuliaji kama namba 9 zenyewe, kama mshambuliaji wa kati, ningemchagua Karim Benzema, Timo Werner, Luis Suarez, Sergio Aguero na Kylian Mbappe.”

Hao ndio washambuliaji bora aliowataja nyota huyo wa kimataifa wa Poland—adui wa magolikipa.

Mchezaji huyo baada ya kumaliza kutaja orodha hiyo, aliulizwa kuhusu mshambuliaji wa klabu yake ya zamani ya Dortmund Erling Haaland ambaye amejiunga na timu hiyo kutoka Salzburg kwenye dirisha dogo mwaka huu.

“ Ana uwezo mkubwa, lakini bado ana muda mwingi wa kukua.” Alisema Lewandoski.

“Sitaki kumpa Pressure kwa maoni yangu”

“Kama atafanya kazi kwa bidii atakuwa ni mchezaji mzuri, na kwa nini asiwe mshambuliaji bora duniani siku moja.”

Lewandowski pia alisema anaona ni bora Haaland aendelee kubakia Bundesliga kwa muda mrefu kabla ya kuchukua hatua nyingine katika maisha yake.

(Visited 770 times, 1 visits today)
Share this post