ASSAs

STAMINA: VIDEO YA KAKA TUCHAT IMEGHARIMU ELFU 60 TU

580
0
Share:

Msanii wa HipHop kutoka kundi la ROSTAM Stamina amesema video ya wimbo wao mpya “Kaka Tuchati” imewagahrimu kiasi cha shilingi elfu 60.

Akizungumza kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV, Stamina amesema idea ya video ya wimbo huo umetoka kwa Director Nicklass ambaye awali aliwaambia anataka kufanya kazi hiyo kila mtu akiwa kwake, pia video hiyo imeshutiwa kwa njia ya simu na sio camera kama ilivyozoeleka.

“Hii video haina bajeti yoyote haizidi elfu 60, gharama nilizozipata ni kuweka bundle na kudownload zile clip, na video yetu haijashutiwa na Camera” amesema stamina

Video hiyo tayari imefikisha jumla ya VIEWS 1.2M hadi muda huu kwenye mtandao wa YouTube na bado inakamata namba 1 kwenye TRENDING TZ kwa siku sita mfululizo tangu iachiwe rasmi Mei 9, 2020.

(Visited 40 times, 1 visits today)
Share this post