ASSAs

ATHARI ZA CORONAVIRUS: CHINA KUTOWEKA LENGO LA UKUAJI UCHUMI MWAKA 2020

49
0
Share:

Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang amesema nchi hiyo haitajiwekea lengo la ukuaji wa uchumi mwaka huu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona

Keqiang amesema wamefikia uamuzi huo kwasababu China itakabiliwa na mambo kadhaa ambayo ni ngumu kutabiri kutokana na kutokuwa na uhakika kuhusu janga la Corona na mazingira ya kiuchumi na biashara duniani

Amesema nchi hiyo inatarajia kukabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi na kutoweka lengo la ukuaji uchumi kutaiwezesha Serikali kuelekeza nguvu zaidi katika kufikia uiamara na usalama

Waziri Mkuu amesema Corona Virus ni changamoto kubwa zaidi ya afya ambayo China imewahi kukutana nayo

Aidha, amesema wataimarisha utaratibu wa afya ya umma, kwa kutoa msisitizo kwenye kujali maisha, kufanya mageuzi ya mfumo wa kukinga na kudhibiti magonjwa, kuboresha mfumo wa utoaji wa tahadhari na taarifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza, kuendelea kutoa habari kwa uwazi kuhusu maambukizi

Serikali imeahidi kuhimiza uzalishaji viwandani na maendeleo ya shughuli mpya zinazojitokeza. Na itaendeleza zaidi mtandao wa Internet na kuhimiza teknolojia ya akili bandia, kwa kimombo “Artificial Intelligence (AI)”

(Visited 7 times, 1 visits today)
Share this post