ASSAs

CHINA KUPITISHA SHERIA ITAKAYOBANA MAANDAMANO HONG KONG

46
0
Share:

Bunge la China linatarajiwa kupitisha sheria ya usalama wa taifa kuhusu Hong Kong, ambayo inaweza kupunguza vuguvugu la upinzani katika eneo hilo lenye mamlaka ya ndani. Hatua hiyo inaashiria azma ya serikali kuu ya China ya kuchukua udhibiti, baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya mwaka jana ya kudai demokrasia Hong Kong.

Hatua hiyo imelaaniwa vikali na Marekani, na huenda ikazua maandamano zaidi mjini humo. Msemaji wa Bunge la China Zhang Yesui amesema bunge litajadili muswada huo katika kikao cha kila mwaka kinachoanza hii leo na kuendelea kwa wiki moja ijayo. Hatua hiyo imekuwa ikizingatiwa kwa muda mrefu na iliharakishwa kufuatia miezi ya maandamano ya kuipinga serikali ya mwaka jana katika koloni hilo la zamani la Uingereza ambalo lilirudishiwa China mnamo mwaka 1997.

(Visited 6 times, 1 visits today)
Share this post