ASSAs

ITALIA KUFUNGUA MIPAKA YAKE KWA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA ULAYA (EU)

51
0
Share:

Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte amesema nchi hiyo itafungua mipaka yake kwa nchi zote ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kuanzia Juni 03 mwaka huu

Conte amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kufufua uchumi na ameeleza kuwa hakutokuwa na utaratibu wa karantini ya lazima kwa wasafiri kutoka nchi wanachama wa EU

Wasafiri kutoka nchi wanachama wa EU hawatokaa karantini lakini wametakiwa kuvaa barakoa na kuzingatia kanuni za umbali ulio salama

Italia imerekodi visa 227,364 vya Corona, wagonjwa 132,282 wamepona hadi kufikia jana na vifo vilivyoripotiwa ni 32,330

(Visited 9 times, 1 visits today)
Share this post