ASSAs

KENYA YAKUMBWA NA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU, 13 WAMEFARIKI DUNIA

45
0
Share:

Wakenya 13 wakiwemo watoto chini ya miaka 10 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu, 12 wametokea Marsabit na mmoja ni kutoka Turkana

Hadi sasa, visa 550 vya Kipindupindu vimerekodiwa na Serikali imesema inafanya jitihada za kudhibiti tatizo hilo ambalo hadi sasa limeripotiwa Kaskazini mwa nchi hiyo

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe amesema wataalamu tayari wanashughulikia mlipuko huo ambao umetokea wakati mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali

Amesema wanaamini inawezekana kudhibiti ugonjwa huo ikizingatiwa kwamba umeripotiwa katika maeneo mawili pekee

(Visited 10 times, 1 visits today)
Share this post