ASSAs

MITIHANI YA KIDATO CHA SITA KUANZA RASMI JUNI 29 MWAKA HUU

36
0
Share:

Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amesema Wanafunzi wa Kidato cha Sita watafungua Shule Juni 01, 2020 na wale wanaosoma Shule za bweni wametakiwa kuanza kuripoti Mei 30

Prof. Ndalichako amesema watakuwa wakijisomea na kufanya maandalizi mpaka Juni 28, 2020. Mitihani ya Taifa itaanza rasmi Juni 29, 2020 na itafanyika hadi Julai 16, 2020. Mitihani hiyo itaenda sambamba na mitihani ya Ualimu

Aidha, Waziri pia ameagiza Baraza la Mitihani (NECTA) kuhakikisha matokeo ya mitihani hiyo yanatoka kabla ya Agosti 31, 2020 ili wanafunzi hao waweze kujiunga na Vyuo Vikuu, kama ambayo Rais ameelekeza

Jana, Rais Magufuli alitangaza Vyuo Vikuu vitafunguliwa Juni 01 mwaka huu, siku ambayo Wanafunzi wa Kidato cha Sita nao watarejea Shule. Hii ni baada ya hali ya Corona nchini kuendelea vizuri

(Visited 6 times, 1 visits today)
Share this post