ASSAs

SUDAN KUSINI: MAMIA WAFARIKI DUNIA KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA

40
0
Share:

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema mamia ya watu wakiwemo wafanyakazi watatu wa kujitolea wameuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotolewa Sudan Kusini

ICRC imesema imekuwa vigumu kuwaondoa marejuhi na kuwahudumia kutokana na uwepo wa taratibu zilizowekwa kwasababu ya Corona. Kamati hiyo imeonya kutakuwa na vifo zaidi ikiwa vurugu zitaendelea

Vurugu zimeongezeka miezi ya hivi karibuni baada ya Serikali kuteua majimbo mapya 10 kumi, lakini ikashindwa kukubaliana juu ya uteuzi wa magavana, jambo ambalo limeleta changamoto katika madaraka

Mifugo na ardhi zimetajwa kama chanzo cha mapigano ya kikabila kwa muda mrefu nchini humo. Mbali na vifo, mapigano hayo pia yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini humo wamelaani vurugu hizo na kuitaka Eerikali kuweka mkakati wa uteuzi wa magavana

(Visited 7 times, 1 visits today)
Share this post