ASSAs

FERGUSON ALIMKATALIA HENRY KUJIUNGA NA UNITED

363
0
Share:

Kiongozi wa ulinzi wa zamani wa Manchester United Ned Kelly amedai kuwa timu hiyo ilikuwa na nafasi kubwa ya kumsajili Thierry Henry kabla ya kwenda Arsenal.

Kwa mujibu wa Kelly, kocha wa muda huo wa Manchester United Sir Alex Ferguson alikataa kumsaini Mfaransa huyo kwa madai kuwa anaandamwa sana na majeraha.

Kelly ambaye licha ya kuwa mkuu wa sekta ya ulinzi wa Manchester United, pia alikuwa ni mlinzi binafsi wa Ferguson, David Beckham na Eric Cantona.

“Tukiwa katika Tunnel baada ya mechi simu yangu iliita, kaka wa Eric (Cantona) Jean-Marie anasema “Ned,mwambie Alex [Ferguson] kuwa Thierry Henry anataka kujiunga na timu” —alisema Kelly katika mahojiano beIN Sports.

“Hii ilikuwa kabla hajaenda Arsenal, chaguo lake la kwanza lilikuwa ni Manchester United. Kwa hiyo nikaenda kwa bosi na kumwambia, ‘bosi ,nilikuwa ninaongea na Jean-Marie Cantona kwenye simu , amesema Henry anataka kujiunga na timu’

“[Ferguson] akajibu, ‘hapana,kila mara huwa anaumia. [Henry] akaenda Arsenal,kilichobaki ni historia”

Thierry Henry akajiunga na Arsenal mwaka 1999 na kwenda kuwa ‘Legend’ wa timu hiyo akifunga magoli 228 na assist 92 kwenye mechi 375 alizocheza, na kuifanya Arsenal kuwa tishio miaka hiyo ya awali ya 2000, ambapo msimu wa 2003-04 walibeba ubingwa wa ligi kuu bila ya kupoteza.

(Visited 40 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us