ASSAs

RATIBA YA LIGI KUU BARA YATANGAZWA, SIMBA NA AZAM KUANZIA DAR

957
0
Share:

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Tanzania Bara, Almasi Kasongo limetangaza michezo ya awali itakayoanza Juni 13, 2020 katika Viwanja tofauti nchini

Tarehe hiyo itakuwa na mchezo kati ya Mwadui FC na Yanga SC katika Uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga na Coastal Union vs Namungo katika Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga

Juni 14, Simba SC itaivaa Ruvu Shooting katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam (haujapangiwa muda) na Azam FC itakutana na Mbao FC katika Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam saa 1 usiku

Almasi amesema wameweka utaratibu wa kuchezwa mechi za mchujo (Play Off) kuanzia tarehe 29 Juni ikiwa ni siku mbili tu baada ya Ligi Kuu kumalizika, mechi za marudiano zitachezwa Agosti Mosi

Michezo ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na Corona

(Visited 197 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us