ASSAs

WATU WAWILI WAMEFARIKI KATIKA MAANDAMANO MAREKANI

999
0
Share:

Watu wawili wamekufa katika mandamano yanayoendelea nchini Marekani kupinga unyanyasaji wa polisi. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu vifo hivyo. Kulingana na duru za vyombo vya habari NBC na CBS vya nchini Marekani, watu wasiopungua sitini wamekwishakamatwa. Visa vya uporaji vimeripotiwa kitongoji cha Cicero mjini Chicago, ambapo maduka kadhaa yamevunjwa. Mjini St.Louis jimboni Missouri, maafisa wanne wa polisi wamepigwa risasi katika maandamano, lakini hawakupata majeraha yanayotishia maisha yao. Bado haijulikani nani amewashambulia maafisa hao wa usalama.

(Visited 160 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us