ASSAs

NJOMBE: MWALIMU AHUKUMIWA KWA KUMJERUHI MWANAFUNZI KWA FIMBO

939
0
Share:

Mahakama ya Wilaya ya Makete imemhukumu Steven Mahenge kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kwenda jela miezi 4 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi Mwanafunzi (13) wa darasa la 7

Februari 18, 2020 katika shule ya msingi Iwale mshtakiwa alimpiga kwa fimbo na mateke mwanafunzi wake (jina linahifadhiwa) na kupelekea kumjeruhi kwa kumvunja mkono

Shtaka hilo ni rufaa iliyokatwa na mlalamikaji kutoka Mahakama ya Mwanzo Matamba baada ya kuona kwamba hakuridhika na hukumu iliyotolewa na Mahakama hiyo ya Mwanzo ambapo alihukumiwa kulipa faini ya Tsh. 100,000 ama kwenda jela miezi 2 pamoja na kumlipa mlalamikaji fidia ya Tsh. 87,000

(Visited 168 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us