ASSAs

SPIKA NDUGAI: MBOWE ALIPELEKWA HOSPITALI AKIWA AMELEWA POMBE

1151
0
Share:

Spika wa Bunge la Jamuhuri wa Muuugano wa Tanzania, Job Ndugai leo Juni 9, ametoa taarifa Bungeni kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alifikishwa hospitalini akiwa amelewa nyakati za usiku.

Amebainisha hayo baada ya Mbunge Joseph Msukuma wakati anachangia hoja kudai kuwa alimuona Mbowe usiku wa kuamkia leo akiwa anakilevi .

”nimetuma madaktari wangu kwenda kule ili kusudi kuzungumza na madaktari wa kule, majibu waliyoniletea nikiwa nimekaa hapa hapa kwamba ni kweli ndugu yetu alifikishwa kule mh. Mbowe kati ya saa nane na saa tisa usiku na walipomfikisha kule alikuwa amelewa chakali ” amesema Spika Ndugai.

Mapema leo Juni 9, 2020 CHADEMA kimeripoti taarifa ya kuvamiwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na watu wasiojulikana akiwa anarejea nyumbani kwake Jijini Dodoma.

(Visited 344 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us