ASSAs

CORONA MAREKANI: MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA YASITISHA MATUMIZI YA HYDROXYCHLOROQUINE

817
0
Share:

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) imesitisha matumizi ya dharura ya dawa ya Malaria ‘Hydroxychloroquine’ kama tiba ya ugonjwa wa Corona

FDA imesema ushahidi mpya kutoka kwenye tafiti zilizofanywa umeonesha hakuna sababu za msingi kuendelea kuamini kuwa dawa hiyo inaweza kutibu Virusi vya Corona

Machi mwaka huu, FDA ilitoa kibali cha dharura kuruhusu Hydroxychloroquine kutumika kwa baadhi ya wagonjwa, lakini tafiti zimeonesha haitibu Corona, na pia ilishindwa kudhibiti maambukizi kwa wale walioitumia

Rais Donald Trump ambaye amekuwa akihamasisha matumizi ya dawa hiyo amesema alizitumia kwa muda wa wiki mbili na hajapata athari yoyote

(Visited 90 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us