ASSAs

TUME YA UCHAGUZI MALAWI YATOA WITO WA AMANI WAKATI KURA ZIKIHESABIWA

333
0
Share:

Tume ya uchaguzi nchini Malawi imetoa mwito wa kudumisha amani wakati kura zikihesabiwa baada ya wananchi kupiga kura kwa mara nyingine ya kumchagua rais Jumanne iliyopita.

Matokeo ya uchaguzi wa kwanza ambapo yalimpa ushindi rais Peter Mutharika yalibatilishwa na mahakama ya katiba kutokana na hitilalafu zilizobainika. . Uamuzi wa mahakama ya katiba nchini Malawi wa kubatilisha ushindi wa rais Mutharika ulisababisha ghasia zilizofanyika kwa miezi kadhaa.

Mutharika amelalamika juu ya vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi na amehoji iwapo matokeo yatakuwa ya kuaminika, wakati huo huo wapinzani nao wanadai kuwa mgombea wao anaongoza.

(Visited 37 times, 1 visits today)
Share this post