ASSAs

BURUNDI YATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

37
0
Share:

Rais mpya wa Burundi Evariste Ndayishimiye ametangaza baraza lake la mawaziri lililopunguzwa, likiwa na mawaziri 15, wengi wao wakiwa maafisa wa utawala huo wenye msimamo mkali kama vile mkuu wa idara inayoogopwa sana ya ujasusi.

Ndayishimiye aliingia madarakni mapema mwezi huu baada ya kifo cha ghafla cha rais wa muda mrefu Pierre Nkurunziza, na wengi walikuwa na matumaini ya enzi mpya baada ya miaka kadhaa ya ukiukaji wa haki za binadamu, ukandamizaji na vurugu.

Hata hivyo, Ndayishimiye ambaye ni jenerali wa jeshi aliyechaguliwa na chama tawala kumrithi Nkurunziza, amewaweka baadhi ya watumishi wenye utata wa utawala katika serikali yake, katika baraza alilolitangaza jana Jumapili.

Wiki iliyopita, Alain-Guillaume Bunyoni, mkuu wa zamani wa jeshi la polisi na waziri wa usalama ambaye aliwekewa vikwazo na Marekani kwa jukumu lake katika ukandamizaji wa kisiasa, aliteuliwa kuwa waziri mkuu.

Kwa mujibu wa tangazo la Jumapili jioni, Gervas Ndirakobuca, mkuu wa idara ya ujasusi, aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Ndirakobuca pia aliwekewa vikwazo na Marekani na pia Ufaransa na Umoja wa Ulaya.

(Visited 11 times, 1 visits today)
Share this post